Utangulizi
Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo
wa Kivenule (KAUKI) iliwasilishwa na Mzee William Sigatambule Kivenule. Mwasilishaji
wa Mada ni Mzee wa Heshima katika Ukoo wa Kivenule ni Tunu kwa sababu ana
madini ya kutosha kuhusiana na masuala ya Ukoo wa Kivenule. KAUKI imekuwa
ikimtumia katika Mikutano yake Kuwasilisha Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo
wa Kivenule.
Katika Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI, Mzee Wiliam Sigatambule Kivenule aliwasilisha Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule. Mwasilishaji wa Mada alianza kwa kuelezea kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule; huku akielezea kwa kina waanzilishi wa Ukoo wa Mwibalama. Mtoa Mada alisema kuwa Ukoo wa Kivenule awali haukuitwa hivyo, uliitwa MWIBALAMA. Kivenule kwa Asili ni akina Balama ni ndugu wa Karibu kabisa ambao hawapaswi hata kuoana.
Picha ya Mzee William Sigatambule Kivenule wa kwanza kutoka kushoto ndiye
aliyewasilisha Mada ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule katika Mkutano Mkuu wa
KAUKI (2024)
CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE
Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka mbali zaidi
hata kabla ya Jina la sasa la KIVENULE kupatikana. Utafiti unaoendelea
kufanyika kila mwaka umesaidia kuboresha Chimbuko la Ukoo wa Kivenule.
Picha inaonesha Vitabu vya Chimbuko na
Muundo wa Ukoo wa Kivenule vilivyoganywa wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI
– Kidamali, Iringa 29 – 30 Juni 2024
Chanzo:
KAUKI - 2024
Waanzilishi Sita (6) wa Ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA)
Kwa mujibu wa Mzee Wiliam Sigatambule Kivenule, wapo Watoto Sita ndio waliopelekea kuanzishwa kwa Ukoo wa Balama. Vizazi hivyo vya akina Balama vilikuja Kumzaa Tagumtwa BALAMA ambaye baadaye ndiye aliyeleta ukoo wa Kivenule. Chimbuko la Mwibalama ni pale Malangali ambayo ipo Kusini mwa Mufindi, katika Mkoa wa Iringa.
Tafiti za sasa zilizopatikana kupitia Mkutano Mkuu wa 13 wa
KAUKI zinaonesha kuwa BABU-------------
ndiye aliyemzaa BABU MWIGINGILI BALAMA; BABU MWIGINGILI BALAMA ndiye alimzaa
BABU MNYARUNGEMBA BALAMA; BABU MNYARUNGEMBA BALAMA ndiye aliyemzaa BABU
NYAKUDILA BALAMA; BABU NYAKUDILA BALAMA ndiye aliyemzaa BABU KANOLO
BALAMA; BABU KANOLO BALAMA ndiye
aliyemzaa BABU MTENGILINGOMA BALAMA; na BABU MTENGILINGOMA BALAMA akamzaa BABU
TAGUMTWA BALAMA.
Picha 2: hazina ya Mashangazi (Sekivenule) kama ilivyochukuliwa katika moja ya matukio yaliyowakutanisha Wanaukoo. Wa pili toka kushoto ni Katibu Mkuu wa Ukoo wa KivenuleChanzo: KAUKI - 2024
Mababu wote hawa tunaowazungumza hapa chini ni Waanzilishi wa UKOO WA BALAMA (akina MWIBALAMA) na Baadaye UKOO WA KIVENULE.
Maelezo haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne ya 17 kabla
ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta Jina la KIVENULE. BABU
MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba Mzazi wa TAGUMTWA BALAMA.
Wakati huu Babu Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda kwenye Vita za
LIGALU.