Hii ni Blog inayomilikiwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kwa ajili kuwahabarisha Ndugu na Wanaukoo, taarifa mbalimbali kuhusu Ukoo wa Kivenule. KAUKI ilianzishwa tarehe 18 Desemba 2005 kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, uliofanyika Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa. Shukrani ziwaendee wote walioshiriki kuanzisha KAUKI: Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule, Ndugu Christian John Kivenule na Ndugu Adam Alphonce Kivenule.
Jumapili, 14 Aprili 2024
UONGOZI WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI) WAWAKUMBUSHA WANAUKOO KUHUSU MKUTANO MKUU
Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya Wanaukoo Wote; wanayofuraha kubwa kuwakumbusha kuwa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI unatarajia kufanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Juni 2024, Kijijini Kidamali, Mkoa wa Iringa. Mkutano huu ni Mwendelezo wa Mikutano ya Ukoo ambayo hufanyika kila Mwaka.
Ili kufanikisha Mkutano huo, Wanaukoo Wote wanaombwa kutoa Michango yao ili kufanikisha Mkutano huo. Watu Wazima Watachangia Shilingi 10,000/- na Watoto 5,000/-. Michango hii itasaidia upatikanaji wa huduma za Chakula, Chai na Maji kwa Siku zote tutakazokuwa Kidamali. Michango itolewe kwa Viongozi wa Kanda Husika.
1. Kutambulishana na Kufahamiana Ndugu/Wanaukoo;
2. Kujua Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
3. Kubadilishana Taarifa na Uzoefu Mbalimbali wa Shughuli
za Maisha;
4. Kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha undugu na
ushirikiano baina ya Wanaukoo; na mengineyo.
Mikutano ya KAUKI huhudhuriwa na Wanaukoo kutoka Maeneo ya Magubike, Kidamali, Kalenga, Nzihi, Nyamihuu, Nyamahana, Nduli, Mgongo, Itagutwa, Igominyi, Vilalo, Migoli, Iringa Mjini, Mafinga, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza na Maeneo mengine ambayo washiriki wanaishi.
Uongozi wa KAUKI
Sambaza kwa Ndugu Wote.
Ijumaa, 27 Oktoba 2023
VIONGOZI WA KAUKI WASISITIZA UMUHIMU WA KUSHIRIKI KATIKA MISIBA YA NDUGU/WANAUKOO
Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) walifanya mazungumzo kuhusu umuhimu wa ndugu/wanaukoo kushirikiana katika misiba na raha. Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Ukoo wa Kivenule Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule alielezea kuhusu taratibu zinazotumika maeneo mbalimbali kuhusu uratibu na ushiriki katika misiba ya ndugu/wanaukoo.
Mwenyekiti alifafanua kuwa jukumu la kuratibu, kushiriki na kusimamia
shughuli za misiba hubebwa na ndugu/wanaukoo waliopo katika eneo ambalo msiba
unakuwa umetokea. Ndugu/Wanaukoo toka maeneo mengine, jukumu lao ni kusaidia
kufanikisha shughuli za msiba huo. Kwa muktadha huo, hata viwango vya ushiriki
katika msiba husika hutofautiana na wahusika waliopo eneo ambako kuna msiba. Lakini
bado wajibu wa kuhakikisha shughuli zinazohusiana na msiba zinafanikiwa ni za
kila ndugu/mwanaukoo.
Jambo la muhimu kuzingatia ni ushiriki wa ndugu/wanaukoo katika matukio
yote ya misiba ya ndugu/wanaukoo; tofauti inayokuwepo ni viwango vya michango
ya rambirambi ili kuweza kufanikisha mazishi ya msiba husika.
Kila maeneo wanatenga viwango vya michango ya rambirambi kwa msiba
unaokuwa umetokea katika eneo husika. Pia kuna viwango vya michango kwa ajili
ya misiba ambayo inakuwa imetokea mbali na maeneo ambayo msiba unakuwa unakuwa
umetokea.
Basi tunasisitiza kuwa ni lazima tushiriki katika misiba yote, ila
viwango vitatofautiana kwa misiba ambayo inakuwa imetokea maeneo yetu
tunayoishi na ile ambayo imetokea maeneo ambayo hatuishi, lakini tuna wajibu wa
kushiriki kwa hali na mali.
Hii itasaidia kupunguza mzigo wa michango kwa sababu kuna wakati
kunakuwa na mfululizo wa misiba…kitu ambacho kinaweza kuwafanya ndugu washindwe
kumudu.
Kwa hiyo, tunaweza kupendekeza viwango vya michango kwa misiba
iliyotokea maeneo ya mbalimbali na tunapaswa kutoa rambirambi zetu.
Kwa ndugu wote tunaoishi Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mafinga,
Mwanza na maeneo mengine tunapaswa kutoa rambirambi kwa msiba uliotokea
Magubike. Tutoe chochote kwa kadri Mungu atakavyokuwa ametujalia.
Suala la Jingine lilikuwa kwenye mjadala ni ushiriki wa misiba kwa
ndugu/wanaukoo. Tulilizungumzia suala la ndugu wengi waliopo Dar es Salaam na
maeneo mengine tofauti na maeneo ya kwetu ambao wana jukumu la kushirikiana
nasi katika shida na raha. Suala la kwenda kwenye misiba maeneo yote, kwa maana
ya Iringa (Nduli, Irore, Kidamali, Magubike, Mufindi, Kalenga, Igominyi, Ilula
na kwingineko ambako ndugu wanaishi) ni muhimu sana kwa kila ndugu/mwanaukoo.
Mwenyekiti alisisitiza umuhimu wa kuwatambua wanaukoo wote na
kuwashirikisha. Pia alipendekeza vikao vya Wanaukoo vitakavyofanyika mwaka huu 2023,
ndugu/wanaukoo waelezwe wazi umuhimu wa kushiriki katika matatizo ya ukoo. Hata
wale ambao tayari wana vikundi vyao watueleze wazi kuwa wao wataendelea
kushiriki kupitia vikundi vyao…au watashiriki pande zote. Hili ni eneo ambalo
pia litakuwa sehemu ya mjadala. Tunaomba ushiriki wa ndugu/wanaukoo uwe mkubwa.
Kikao kwa upande wa Dar es Salaam kimepangwa kufanyika mwaka
2023….Onesmo Bernard Kivenule atatupatia mwongozo wa wapi kikao kitafanyika.
Kifupi ni haya ambayo yamekuwa sehemu ya mujadala.
Nawasilisha.
Asante
Imetolewa Oktoba 2023
Jumatatu, 2 Oktoba 2023
MATUKIO MUHIMU KATIKA PICHA - UMOJA WA UKOO WA KIVENULE - KAUKI
Ni picha matukio mbalimbali wakati wa Msiba wa Marehemu Stewart Edgar Kivenule. Hapa ni eneo la Mlafu katika Maziko ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI). Tarehe 7 Septemba 2023
Picha za Wajukuu wa Sigatambule Kivenule













