Hii ni Blog inayomilikiwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kwa ajili kuwahabarisha Ndugu na Wanaukoo, taarifa mbalimbali kuhusu Ukoo wa Kivenule. KAUKI ilianzishwa tarehe 18 Desemba 2005 kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, uliofanyika Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa. Shukrani ziwaendee wote walioshiriki kuanzisha KAUKI: Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule, Ndugu Christian John Kivenule na Ndugu Adam Alphonce Kivenule.
Jumatano, 28 Mei 2025
MIKUTANO YA KAUKI
|
1.1.1.
Historia Ya
KAUKI Umoja wa Ukoo
wa Kivenule (KAUKI), ulianzishwa rasmi tarehe 18 Desemba 2005 wakati wa
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa KAUKI uliofanyika Kijijini Kidamali. KAUKI
ilianzishwa kutokana na mashauriano ya Ndugu watatu, yaani Faustino
Sigatambule Kivenule, Christian John Kivenule na Adam Alphonce Kivenule. Ndugu hawa
watatu baada ya kubaini mapungufu katika Nyanja ya Mahusiano, Ushirikiano na Kufahamiana
miongoni mwa ndugu na wanaukoo kwa ujumla ndani ya Ukoo wa Kivenule, waliamua
kuungunisha nguvu zao na kisha kuushirikisha ukoo kuhusiana na adhima yao ya
kutaka kuirudisha jamii ya ukoo wa Kivenule kuwa pamoja. 1.1.2. Mikutano ya Mashauriano Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Mashauriano ulifanyika Jijini Dar es Salaam, mnamo tarehe 06
Februari 2005 katika Ukumbi wa Riverside uliopo eneo la Ubungo, ambapo ndugu
zaidi ya 15 walihudhuria. Matokeo ya Kikao hiki yaliazimia kwa kauli moja,
kulishirikisha wazo la kuandaliwa kwa MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA
KIVENULE, kwa ndugu zao wanaoishi maeneo ya Magubike, Kidamali, Nyamihuu,
Ilalasimba, Idete, Ibogo, Nzihi na Iringa Mjini. Kukubalika
kwa wazo hili ndiko kulikopelekea kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule, mnamo tarehe 17 -18 Desemba 2005, Kijijini Kidamali, Mkoani
Iringa. 1.1.3.
Idadi ya Mikutano
ya KAUKI iliyokwishafanyika Mara baada ya
kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, pamekuwepo na
mwendelezo wa kuendelea kufanyika kwa mikutano hiyo. Tokea wakati huo,
Mikutano ya KAUKI imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa kuzingatia maeneo ya
Kanda. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa, Mikutano 12 ya KAUKI imefanyika maeneo
mbalimbali ya Kanda za KAUKI kama inaoneshwa hapa chini: 1. Kanda ya Kidamali –
Mikutano ya KAUKI 5 2. Kanda ya Magubike –
Mikutano 2 3. Kanda ya Irore – Mkutano 2
na Mkutano 1 ukiwa umefanyika eneo la Vilalo 4. Kanda ya Nduli – Mkutano
1 5. Kanda ya Mufindi –
Mkutano 1 6. Kanda ya Dar es Salaam –
Mkutano 1 Kwa KAUKI haya ni matokeo ya Kujivunia kwa sababu siyo rahisi kufanyika kwa mikutano ya namna kutokana na kuandaliwa kwa gharama kubwa. 1.1.4. Mafanikio Ya KAUKI KAUKI
imefanikiwa kufanya yafuatayo kwa maendeleo ya wana-ukoo. Kwa mfano, Imeanzisha
Blogu zake kwa ajili ya upashanaji habari. Anuani za blogu hizo ni: https://tagumtwa-kivenule.blogspot.com/ https://adamkivenule.blogspot.com/2013/ http://www.kauki-kauki.blogspot.com/ Pia ukiingia kwenye ukurasa wa Google unaweza kuandika Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule au Kuandika neno Kivenule tu…utapata taarifa za kutosha za Ukoo wa Kivenule, zikiwemo blogs na YOUTUBE. Hali kadhalika, blogu inayomilikiwa na ndugu Adam Kivenule, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa KAUKI imekuwa ikisaidia katika suala nzima usambazaji na upashanaji wa habari za KAUKI. Anuani ya blogu hiyo ni: https://adamkivenule.blogspot.com/ KAUKI pia imefanikiwa kufungua Ukurasa wa Facebook wenye anuani ifuatayo: https://www.facebook.com/kivenule/ KAUKI pia imefungua ukurasa wa TWITTER http://www.twitter.com/kivenule Taarifa za
KAUKI zipo YOUTUBE unaweza kuingia Youtube na kuandika Ukoo wa Kivenule au
Kuandika TAGUMTWA. Hali
kadhalika, unaweza kuwasiliana na viongozi wa KAUKI au ofisi ya KAUKI kwa
kutumia baruapepe zifuatazo: Au unaweza kutuma taarifa kuhusiana na ukoo wa Kivenule moja kwa moja kwenye Blog yetu ya Tagumtwa-Kivenule kwa kutumia barua-pepe ifuatayo: |
Jumatatu, 26 Mei 2025
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI - KIDAMALI, IRINGA 2024
| Picha inaonesha Ukumbi uliotumika katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) |
| Mzee William Sigatambule Kivenule (kushoto) akiwa na Bi. Happy Xavery Kivenule wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI |
| Wanaukoo mbalimbali wakipata chakula wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI - 2024 |
| Mwenyekiti wa KAUKI akiwa na Mzee William Sigatambule Kivenule ambaye amekuwa akitoa Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule |
| Wanaukoo wakiwa katika Usiku Maalum wa KAUKI - Kidamali Iringa. Hii ilikuwa ni wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI |
| Bango kuonesha Kaulimbiu ya Ukoo wa Kivenule iliyozinduliwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI |
V
| Wanaukoo wakiwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI uliofanyika Kijijini Kidamali - Iringa Vijijini |
| Shangazi Anyesi Sigatambule Kivenule kutoka Kanda ya Magubike, naye alikuwa sehemu ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI |
| Wanaukoo wakiwa tayari kuingia kwenye Mkutano wa 13 wa KAUKI |
| Wanaukoo wakibadilisha mawazo wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI |
| Picha ya Kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI. Hawa ni baadhi ya wanaukoo waliohudhuria Mkutano huo. |
RATIBA YA MKUTANO MKUU WA 14 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
|
https://tagumtwa-kivenule.blogspot.com/ RATIBA YA MKUTANO
MKUU WA 14 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)-KIDAMALI - IRINGA |
||
|
Siku ya Kwanza: JUMAMOSI 21 JUNI
2024 |
||
|
MUDA |
SHUGHULI/JUKUMU |
MHUSIKA |
|
12.00-01.00 Asb. |
|
Ndugu/Wanaukoo Wote |
|
01.00-02.00 |
Kupata Kifungua Kinywa (Chai/Kahawa/Uji) |
·
Ndugu Wote ·
Kamati ya Maandalizi |
|
02:00-02:50 |
1.
Kukaribisha Wageni 2.
Kujisajili/Orodhesha
Washiriki 3.
Kuwapa Vitambulisho |
·
Kamati ya Maandalizi ·
Washiriki Wote |
|
02:50-02:55 |
Dua/Sala ya Kuombea Mkutano |
·
Viongozi wa Dini |
|
02:55-03:00 |
Salaam toka Kanda ya Kidamali: Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu 14 wa
KAUKI |
·
Mwakilishi Kanda ya Kidamali |
|
03.00–03.05 |
Neno fupi la Kumkaribisha na Kumtambulisha Mgeni Rasmi |
·
Mwenyekiti wa KAUKI |
|
03.05-03.25 |
Hotuba ya Ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI |
·
Mgeni Rasmi |
|
03.25-04.00 |
Utambulisho wa Ndugu na Wageni Waalikuwa |
·
Mwenyekiti-KAUKI ·
Washiriki Wote |
|
04.00-05:00 |
MADA: Chimbuko/Asili Na Historia Ya Ukoo Wa Kivenule 1.
Mjadala: Muundo wa Ukoo wa Ukoo wa Kivenule (Nakala Zisambazwe) |
·
Mtoa Mada ·
Viongozi-KAUKI ·
Washiriki wote |
|
05:00-05:30 |
Pumziko la Chai / Kahawa/Maji |
Washiriki Wote |
|
05.30-07.00 Mchana |
Mada Inaendelea… 2.
Namna ya Kuiboresha Mada: Mapendekezo 3.
Nini kifanyike kutunza kumbukumbu za Ukoo 4.
Njia Mbadala za Kutunza Taarifa za Ukoo |
·
Viongozi-KAUKI ·
Wawezeshaji ·
Washiriki wote |
|
Majumuisho |
·
Viongozi wa KAUKI |
|
|
07.00-08.00 |
CHAKULA CHA MCHANA |
Washiriki wote |
|
08:00-08:40 |
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KANDA Nafasi: 1.
Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti 2.
Katibu na Naibu Katibu 3.
Mweka Hazina/ Walezi wa
Kanda, Wahamasishaji |
1. Kanda ya DAR 2. Kidamali/Magubike 3. Kalenga/Irore 4. Nduli/Morogoro 5.
Dodoma/Mafinga |
|
08.40 – 09.20 Alasiri |
Maendeleo ya KAUKI Katika Kanda: 1.
Hamasa, Mafanikio 2.
Changamoto na Mikakati |
·
Viongozi wa Kanda ·
Ndugu toka Kanda Husika |
|
9:20 – 9:45 |
Hali ya Ukoo/KAUKI: Maendeleo kwa Ujumla;Changamoto;Ushauri na
Mapendekezo |
·
Viongozi wa KAUKI ·
Wanaukoo Wote |
|
09:45-10:00 |
Salaam mbalimbali kwenye
Mkutano Mkuu 14 wa KAUKI (Wastani watu 6 @ dakika 2) |
·
Washiriki wa Mkutano |
|
10.00-10.45 Jioni |
Kuahirisha
Mkutano hadi Siku ya Jumapili tarehe 21 Juni 2025 |
·
Mwenyekiti – KAUKI ·
Washiriki Wote |
|
02:00 - 06:00 Usiku |
NDUGU KUJUMUIKA PAMOJA (KAUKI NIGHT GALA)
kwa ajili ya Vinywaji na Nyama Choma |
Ndugu Wote Kamati ya Maandalizi |
|
RATIBA YA MKUTANO
MKUU WA 14 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)-KIDAMALI - IRINGA |
||
|
Siku ya
Pili: JUMAPILI 22 JUNI 2024 |
||
|
MUDA |
SHUGHULI/JUKUMU |
MHUSIKA |
|
12.00-01.00 Asb. |
|
Ndugu Wote |
|
04.00-05.00 |
Kupata Kifungua Kinywa (Chai/Kahawa/Uji) |
·
Ndugu Wote ·
Kamati ya Maandalizi |
|
05:00-06:00 |
MADA YA II: ELIMU YA UJASILIAMALI - 1 ·
Uwasilishaji ·
Mjadala ·
Majumuisho |
·
Mwezeshaji ·
Washiriki Wote |
|
06:00-07:00 |
MADA YA III: ELIMU YA UJASILIAMALI - 2 ·
Uwasilishaji ·
Mjadala ·
Majumuisho |
·
Mwezeshaji ·
Washiriki Wote |
|
07:00-08:00 |
MAPUMZIKO YA
CHAKULA CHA MCHANA |
·
Washiriki Wote |
|
08.00–09.00 Alasiri |
MADA YA IV: ELIMU YA UJASILIAMALI - 3 ·
Uwasilishaji ·
Mjadala ·
Majumuisho |
·
Mwezeshaji ·
Washiriki Wote |
|
09.00-09.30 |
·
Majumuisho ya Mkutano Mkuu wa 14 wa KAUKI ·
Maazimio |
·
Viongozi wa KAUKI ·
Washiriki Wote |
|
09.30-09.40 |
·
Neo la Shukrani Toka Kamati ya Maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa 14 wa KAUkI - Kanda Ya Kidamali |
·
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi |
|
09.40-09:50 |
Neno la Shukrani toka kwa Viongozi wa KAUKI |
·
Viongozi wa KAUKI |
|
09:50-09:55 |
KUTANGAZA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA 15 WA
KAUKI NA MAHALI UTAKAPOFANYIKIA |
·
Mwenyekiti – KAUKI ·
Washiriki Wote |
|
09:55.00-10.00 Jioni |
Kuahirisha
Mkutano Mkuu wa KAUKI - 2025 |
·
Mwenyekiti – KAUKI |
|
10:00 |
MWISHO |
Ndugu Wote Kamati ya Maandalizi |

