Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) ulifanya kikao cha
dharura cha masaa matatu (3) tarehe 7 Septemba 2023 siku ya Alhamisi, Kijijini
Kidamali baada ya kuhitimisha mazishi ya ndugu yetu Steward Edgar Kivenule.
Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UKOO wa
Kivenule Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule; na kilihudhuriwa na Wanaukoo
wengi waliohudhuria mazishi ya Marehemu Stewart Edgar Kivenule.
Agenda Kuu ya Kikao hicho ilikuwa ni kujadili
changamoto zilizosababisha kutoendelea kufanyika kwa Mikutano ya UKOO. (Taarifa
Rasmi itatolewa).
Aidha UKOO wa Kivenule kupitia Mkutano huu umeazimia
kwa Pamoja kuendelea kufanya Mikutano ya UKOO wa Kivenule.
Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ujao umepangwa
kufanyika Tarehe 29 ya Juni 2024 Kijijini Kidamali. Lengo la kufanyika Kidamali
ni kuendelea kuongeza hamasa kwa Wanaukoo wote, na hasa ikizingatiwa kuwa
Kidamali kuna mkusanyiko mkubwa wa ndugu.
Kabla ya kufanyika kwa Mkutano huo, kutakuwa na Vikao
vya Utangulizi kwa Viongozi wa Kanda mbalimbali ili kuweza kuwasilisha taarifa
na pia kuweka mikakati ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Mwaka 2024.
Imetolewa na Uongozi wa KAUKI

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni