Toleo la Kwanza - 2013
UKOO NI NINI?
Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani. Unaweza
kuwa utambulisho wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Utambulisho wowote kati ya
hizo nilizotaja, unaufanya ukoo utambulike miongoni mwa jamii mbalimbali. Mara
nyingi utambulisho ambao huufanya ukoo utambulike baina ya jamii za Kiafrika ni
Jina. Pamoja na jina, halikadhalika kuna tunu (values) mbalimbali ambazo
huheshimiwa na ukoo husika na jamii kwa ujumla.
Tunu hubeba mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miiko, maadili, heshima, vyakula na tamaduni. Sambamba na tunu, pia kuna Mila na Desturi, ambazo huzingatiwa sana katika masuala ya kijamii, mfano wakati wa kuoa au kuoza, misiba, sherehe za jadi mfano matambiko na masuala ya kimila.
Ukoo wa Kivenule ni mmojawapo wa koo nyingi kubwa zilizopo katika Himaya ya Uhehe katika Mkoa wa Iringa. Ukoo wa Kivenule ulianza kutambulika toka Karne ya 18. Historia inaonesha kuwa Ukoo huu asili yake ni kutoka kwa Wabena-Manga, waliopo Kusini mwa Mji wa Iringa; yaani maeneo ya Mufindi na Njombe. Ni mchanganyiko wa Wahehe na Wabena wanaojulikana kama Wabena-Manga.
Wahehe ni moja kati ya makabila makubwa hapa Tanzania ambalo kiasili linaishi katika Wilaya za Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa, yaani Iringa Vijijini, Iringa Mjini, Kilolo na Mufindi. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazopatikana na kutafitiwa, inasemekana kuwa ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji; yaani Wahehe wenye Asili ya Ungazija. Pengine hata ile sababu ya kuzika wafu wao wakielekea mashariki inapewa uzito.
Katika kuenzi na kutunza tunu za asili za Uhehe, Ukoo wa Kivenule hauli
nyama ya Mbawala (kwa lugha ya Kihehe Mato/Imato). Imani kubwa imejengeka
miongoni mwa jamii ya Ukoo wa Kivenule kuwa kula Mbawala ni kuvunja miiko ya
Ukoo ambayo iliyowekwa na Waasisi wetu (Babu zetu). Mara mwanaukoo anapokiuka
miiko hii na kula nyuma ya Mbawala (Imato) basi huweza kufikwa na matatizo
mbalimbali, mfano kudhurika afya yake. Mara nyingi huwapata matatizo kama ya
kuvimba miguu na pengine kuoza kabisa.
Tunu nyingine ambazo Ukoo wa Kivenule unazienzi kama zilivyo koo
nyingine katika Uhehe ni Miitikio (Midikiso). Tunu hii huutambulisha
Ukoo wa Kivenule miongoni mwa Koo za Wahehe. Mwitikio (Mwidikiso) wa Ukoo wa
Kivenule ni 'MLIGO'. Mwitikio huu hutumika katika maeneo mbalimbali
mfano katika salamu, kuapa (kufanya viapo) na pia kujitofautisha na koo
nyingine. Miitikio (Midikiso) huutambulisha Ukoo wa Kivenule katika koo
nyingine katika ardhi ya Uhehe.
CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE
Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka
mbali zaidi hata kabla ya Jina la sasa la KIVENULE kupatikana. Utafiti
unaonesha kuwa BABU NYAKUDIRA BALAMA ndiye aliyemzaa (Baba
yake) BABU KANOLO BALAMA. Hapa tunauangalia Ukoo wa Balama.
Hali kadhalika, BABU KANOLO BALAMA, akamzaa BABU
MTENGELINGOMA BALAMA. Maelezo haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne
ya 17 kabla ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta Jina
la KIVENULE.
BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba
Mzazi wa TAGUMTWA BALAMA. Wakati huu Babu Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda
kwenye Vita za LIGALU.
Kwa Asili, Ukoo wa Balama na baadaye
Kivenule ni maarufu kama Wapiganaji wa Vita. Ukoo wa Balama (Kivenule) ulikuwa
hodari sana katika vita vya msituni ambavyo viliwahusisha Babu zetu akina TAGUMTWA.
Enzi hizo za Mababu zetu vita za Koo na Kabila zilipiganwa maeneo mengi ya
himaya ya Uhehe kwa lengo la kupata mali, mifugo na heshima.
Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE)
ndiye aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Babu
KALASI KIVENULE. Ikumbukwe kuwa, jina halisi la ukoo wa Kivenule ni BALAMA.
Kama ilivyokwisha julikana katika mada zilizowasilishwa katika Mikutano Mikuu
Tisa ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha
sifa ya kuwa jasiri Vitani na hasa katika kutumia silaha
za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha Asilia
ya Kihehe “KUMIGOHA”. Yaani kwa maana nyingine LIGALU yenye
maana ya Kwihoma Imigoha – Kuhoma
Vatavangu au Kuvenula Avatavangu. LIGALU maana
yake Vita. Kuhoma maana yake Kuchoma na Migoha maana
yake Mikuki. Venula maana yake ua, fyeka
maadui.
LIGALU ndiyo
iliyochangia kuzaliwa kwa jina la Ukoo la KIVENULE. KIVENULE maana
yake ni Ushujaa kutokana na Shabaha ya Mikuki.
KUVENULA likiwa na maana
halisi ya kuwa na shabaha ya kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale
na Mikuki. Babu zetu akina TAGUMTWA BALAMA walilidhihirisha
hili katika Vita na Watavangu na hivyo kusababisha kuzawadiwa kwa jina la KIVENULE kama
jina la sifa kutokana na ushujaa katika Vita.
Tagumtwa Balama asili
yake ni kutoka katika Ukoo wa Balama. Sifa kubwa ya Tabu Tagumtwa, alikuwa ana
Shabaha sana ya Mikuki katika uwanja wa Vita. Alikuwa hakosei shabaha (target)
na hivyo hupelekea kuwaangamiza na kuwaua sana maadui. Wakati
akiwamaliza/fyeka/kuwaua adui zake kwa Mikuki, Wakuu wa Vita (Vatavangu)
walikiita kitendo hicho 'KUVENULA'. Taarifa za Tagumtwa kuua (Kuvenula)
adui zake katika uwanja wa vita, zilizagaa kila mahali na hivyo kupelekea Wakuu
(Viongozi) wa Vita (Vatavangu) kumzawadia Jina la KIVENULE, kama
jina la sifa na heshima kwa kuwa shujaa wa Vita.
Ikumbukwa kuwa asili ya Ukoo wa
Kivenule ni kutoka katika ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA). Hawa ni ndugu
wa karibu wa Kivenule kabisa na hawapaswi kuoana. Koo za Mwibalama zinapatikana
maeneo mengi katika Mkoa wa Iringa hususani katika Wilaya za
Mufindi, Iringa Vijijini, Iringa Mjini na Kilolo; hali kadhalika kama ilivyo
ukoo wa kina Mwakivenule.
TAGUMTWA KIVENULE alifia katika
uwanja wa mapambano (vita) na mwili wake haukuweza kupatikana. Kama zilivyo koo
za machifu au watu maarufu miili yao ilikuwa haizikwi. Baada ya kufa
iliegemezwa kwenye miti mikubwa na kuliwa na wanyama. Wakija watu wasiukute
mwili basi huamini kuwa mwili umechukuliwa na Mungu.
KUKUA NA KUZAGAA KWA UKOO WA KIVENULE
Kwa mujibu wa taarifa mbalimblai za
kitafiti ambazo zimekuwa zikifanyika toka mwaka 2005 hadi sasa 2013; kupitia
mikutano mbalimbali ya KAUKI; zinabainisha kuwa,
BABU NYAKUDIRA
BALAMA alimzaa BABU KANOLO BALAMA. Hali kadhalika BABU KANOLO BALAMA
alimzaa MTENGELINGOMA BALAMA. BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye aliyemzaa
Tagumtwa Balama (Kivenule).
Baada ya hapo, tunaona sasa Kizazi
cha TAGUMTWA KIVENULE kinaanza kujitokeza. Hii ilikuwa ni
Karne ya 18. TAGUMTWA KIVENULE alizaa watoto wawili (2). Bado
utafiti unafanyika kumfahamu Mama wa watoto hawa. Watoto wa Tagumtwa Kivenule
walikuwa ni TAVIMYENDA KIVENULE na KALASI KIVENULE. Kwa mujibu wa
taarifa kadhaa tulizonazo kwa sasa; hawa ni vinara wa Ukoo wa Kivenule ulioenea
maeneo mbalimbali hapa Tanzania.
Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule
katika harakati za kutafuta maisha walifika katika eneo la Kalenga, mahali
alipoishi Mkwawa na kukutana na na Mwamyinga, aliyekuwa mfugaji maarufu katika
eneo la Ulefi huko Magubike, Iringa Vijijini. Tavimyenda Kivenule alibahatika
kupata kazi kwa Mwa-Myinga baada ya kuombwa kwenda kumwangalizia mifugo yake
huko Magubike, huku akimwacha mwenzake Kalasi pale Kalenga.
Kalasi Kivenule yeye hakupata fursa
hiyo ya kazi na hivyo akaamua kuelekea eneo Irore katika Wilaya Iringa Vijijini
(kwa sasa Kilolo) kutafuta maisha. Huu ukawa ni mwanzo wa kugawanyika kwa
watoto hawa wawili wa Tagumtwa Kivenule.
Tavimyenda Kivenule akielekea upande wa
Magharibi mwa Mji wa Iringa na Kalasi alielekea upande wa Mashariki mwa Mji wa
Iringa.
Historia inabainisha kuwa pamoja na
Babu hawa kugawanyika kutokana na utafutaji wa maisha, mahusiano na ushirikiano
baina yao haukuvunjika. Babu zetu waliendelea kushirikiana na kutembelea licha
ya ukoo kukua na kuwa mkubwa sana.
KIZAZI CHA TAVIMYENDA KIVENULE
Katika Karne ya 19 hadi 20, Kizazi cha
Tavimyenda Kivenule kilizaliwa na kuzagaa katika maeneo ya Ulefi, Magubike na
Mlafu, Wilaya ya Iringa Vijijini, Iringa Mjini na maeneo mengine mkoani Iringa.
Taarifa tulizonazo kupitia tafiti
tunazofanya, hali inaonesha kuwa, Babu Tavimyenda alikuwa na wake watatu (3),
ambao ni:
1. Bibi Mkami Sekabogo
2. Bibi Senosa
3. Bibi Pili Mvemba
Mke wa kwanza wa Tavimyenda Kivenule
aliolewa akiwa na mtoto; aliyejulikana kama Bibi Sikimbilavi Semabiki. Kwa mke
huyu wa Kwanza Sekabogo, Tavimyenda alizaa nae watoto wanne (4); ambao ni:
1. Babu Kavilimembe Kivenule
2. Babu Mgaifaida Kivenule
3. Babu Sigatambule Kivenule
4. Babu Hussein Kivenule
(Bado yupo hai)
Kwa Mke wa Pili Bibi Senosa, Babu
Tavimyenda akizaa nae watoto watatu (3); ambao ni:
1. Babu Abdallah Kivenule
2. Bibi Sigungilimembe Kivenule
3. Bibi Malibora Kivenule
Watoto hawa wa Bibi Senosa waliishi
maeneo ya Kihesa katika Mji wa Iringa.
Kwa upande wa mke wa Tatu wa Bibi Pili
Mvemba; Babu Tavimyenda alizaa mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI
KIVENULE aliishi eneo la Ulefi. Baada ya kufariki amezikwa Mlafu. Babu
Tavimyenda Kivenule amezikwa katika eneo la Ulefi.
Bibi SIKIMBILAVI alikuwa mtoto
wa kufikia wa Bibi MKAMI SEKABOGO. Bibi SIKIMBILAVI aliolewa
na Ukoo wa Mgoda na kubahatika kupata watoto wanne (4) ambao ni:
1. Mama wa
Kitatambe
2. Salia Maneno Mgoda
3. Galamale
Mgoda
4. William Mgoda
Baada ya hapo kizazi hiki kimeendelea
kukua hadi hivi sasa Karne ya 21. **Angalia Chati kuonesha Muundo wa Ukoo wa
KIVENULE**
KIZAZI CHA KALASI KIVENULE
Kwa upande wa Kalasi Tagumtwa Kivenule,
kizazi hiki kilienea maeneo ya Nduli, Mgongo, Itagutwa, Kigonzile, Igominyi na
Irore. Taarifa zinaonesha kuwa, Babu Kalsi Kivenule alikuwa na wake wawili (2);
yaani:
1. Bibi Semsakwa Mnonikilwa
2. Bibi Mnyamtage Sekindole
Bibi Semsakwa Mnoni Kirwa kwa Babu
Kalasi Kivenule alizaa watoto wawili (2) ambao ni:
1. Bibi Cheilaje
Nginasambula Kivenule
2. Gingilemesa
Kivenule
Kwa bahati mbaya hakuna taarifa zozote
za hawa watoto wawili wa Kalasi.
Kwa upande wa Bibi Mnyamtage Sekindole,
Babu Kalasi Kivenule alizaa mtoto mmoja ambaye ni Salamalenga Kahengula
Kivenule. Bibi Mnyatage Sekindole awali alikuwa ameolewa kwa Mwa-Mhumba na
kuzaa nae mtoto mmoja aliyeitwa Bibi Mganga Semhumba na baadaye kufariki. Baada
ya hapo aliolewa na Kalasi ambapo pia alizaa mtoto mmoja tu anayefahamika kwa
jina la Salamalenga Kahengula Kivenule. * Angalia watoto wa Kahengula katika
Chati ya Muundo wa Ukoo wa Kivenule*
Kuna taarifa nyingi kutoka kwa Babu
Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule. Mwingiliano wa koo nao unaonesha
simulizi hizi. Kwa upande wa Tavimyenda mke wa Kwanza Bibi Mkami Sekabogo
alikuwa na mtoto wa kufikia, aliyejulikana kwa jina la Bi Sikimbilavi Semabiki.
Hatujapata taarifa rasmi kuhusiana na kizazi cha Bibi huyu, kama ilivyotokea
kuwa Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi aliyekuwa mtoto wa kufikia Bibi
Semkonda mke wa Salamalenga Kahengula Kivenule.
Sipanganakumtwa Mwilongo Regiona
Sematagi amesaidia kueneza kizazi cha Ukoo wa Mnyavanu. Taarifa zaidi na ukoo
wa Mnyavanu upo katika Chati ya Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule.**
TABIA YA KIZAZI CHA TAVIMYENDA NA
KALASI KIVENULE KUOA WAKE WENGI
Tabia nyingine ya kizazi hiki cha
Tavimyenda na Kalasi ilikuwa ni kuoa wake wengi. Kwa mfano Tavimyenda pekee
alikuwa na wake watatu. Hali kadhalika Kalasi naye alikuwa na wake wawili.
Hali hii ya kuwa na mke zaidi ya mmoja
walirithi watoto wao. Kwa mfano watoto watatu wa kiume wa Tavimyenda
waliozaliwa kwa Bibi Mkami Sekabogo walioa wake wawili hadi watatu. Mtoto wa
kwanza wa Babu Tavimyenda Kivenule aliyejulikana kama Kavilimembe Kivenule
alikuwa na wake wawili (2). Mtoto wa tatu wa Bibi Mkamai Sekabogo,
aliyejulikana kwa jina la Sigatambule Matesa Kivenule, alikwa na wake watatu.
Hali kadhalika mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo anayejulikana kama Hussein
Kivenule alikuwa na wake wawili. Mtoto pekee wa Pili wa Bibi Mkami hakubahatika
kuwa na familia; na alijiita jina la kujinyanyapaa "Mgaifaida"
Kivenule.
Sambamba na tabia ya Ukomo wa Kivenule
kuoa mke zaidi ya moja; pia kuna utamaduni uliojitokeza kwa baadhi ya watoto wa
Bibi Mkami Sekabogo kuoa dada na mdogo wake. Hili linajidhihirisha kwa wake
wawili wa Babu Kavilimembe Kivenule ambao walikuwa ni Bibi Sikumwendinguluvi
Sekusiga (Bi Mkubwa) na Bibi Gakumwalia Sekusiga (Bi Mdogo).
Hali kadhalika kwa mtoto wa tatu wa
Bibi Mkami Sekabogo; Babu Sigatambule Matesa Kivenule alioa wake watatu, ambapo
wake wawili wakubwa, 'Bibi Sikumwendinguluvi Singaile (Bi Mkubwa) na Bibi
Nyanyilemale Singaile (Bi Mdogo wa Pili); na wa tatu aliitwa Bibi Pangulimale
Setwanga.
Mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo
Hussein Kivenule, yeye alioa wake wawili kutoka familia tofauti. Wake zake
waliitwa Bibi Yimilengeresa Semsisi (Bi Mkubwa) na Bibi Dalika Setala (Bi
Mdogo). Kwa upande wa watoto Kalasi Kivenule, mtoto wake Salamalenga Kahengula
Kivenule naye alioa wake watatu; ambao ni Bibi Semkonda, Bibi Semfilinge na
Bibi Nyangali.
Hatujapata taarifa rasmi za watoto wa
Kalasi kutoka kwa mke wake Bibi Semsakwa Mnonikilwa ambao ni Cheilaje
Nginasambula Kivenule na Gingilemesa Kivenule. Kwa upande wa Kahengula yeye
alioa kutoka katika familia tofauti.
UZAO WA BABU KAVILIMEMBE, MGAIFAIDA,
SIGATAMBULE NA HUSSEIN KIVENULE
Babu Kavilimembe Kivenule aliishi eneo
la Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, huku akipakana na Ulefi upande wa
Kaskazini, Idete na Ibogo upande wa Magharibi. Akiwa ameoa wake wawili wa
familia moja, Babu Kavilimembe alibahatika kupata watoto sita (6).
Kwa upande wa mke wa kwanza Bibi
Sikumwendinguluvi Sekusiga; Mzee Kavilimembe Kivenule alipata watoto wafuatao:
1. Elizabert Kivenule
2. Dalikimale Kivenule
3. Sandra Kivenule
4. Pangalasi Kivenule
Na kwa mke mdogo Bibi Gakumwalia
Sekusiga, Mzee Kavilimembe alipata watoto wawili ambao ni:
1. Salikuvaganga Kivenule
2. Francis Kivenule
Watoto hao wa Babu Kavilimembe wengi
wao waliishi maeneo ya Ulefu na Magubike. Baadhi yao walihamia maeneo mengine
kama Nzihi, ukiacha wale waliokuwa watumishi wa serikali wakaenda kuishi maeneo
mbalimbali. Babu Kavilimembe amezikwa eneo la Magubike, Iringa Vijijini.
Kwa upande wa Babu Mgaifaida (Yakobo)
Kivenule, yeye hakubahatika kupata familia. Mgaifaida alikuwa na ulemavu ambao
ulimfanya ashindwe kutembea katika hali ya kawaida. Muda mwingi aliishi eneo la
Ulefu kabla ya sehemu kubwa ya Ukoo wa Kivenule kuhamia sehemu ya Mlafu. Baada
ya kufariki, alizikwa Mlafu.
Babu Sigatambule Matesa Kivenule
alikuwa ni mtoto wa tatu wa Tavimyenda Kivenule kwa Bibi Mkami Sekabogo. Babu
Sigatambule aliishi Ulefi, akahamia Mlafu na baadaye Kidamali. Babu Sigatambule
ndiye aliyehakikisha Ukoo wa Kivenule unapata eneo la Mlafu huku akipambana na
Wagiriki. Walowezi na wawekezaji katika zao la Tumbaku.
Babu Sigatambule Kivenule katika uhai
wake alibahatika kuoa wake watatu (3); huku wake zake wawili wakitoka katika
familia moja ya ukoo wa Singaile. Wake zake hawa wakubwa waliitwa Bibi
Sivangumhavi Singaile na Bibi Nyanyilimale Singaile. Mke wa Tatu wa Babu
Sigatambule aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga. Wote waliishi Mlafu na baadaye
kuhamia eneo Kidamali.
Wake zake wawili Bibi Nyanyilimale
Singaile na Bibi Pangulimale Setwanga bado wapo hai na wanaishi Kidamali mpaka
leo.
Watoto wa Babu Sigatambule Kivenule ni
hawa wafuatao:
Kwa Bibi Sivangumhavi Singaile (Mke
Mkubwa):
1. Gidagumhindi Cecilia Kivenule
2. Semyamba Khadija Kivenule
3. Sivinitu Alphonce Kivenule
4. Kadungu William Kivenule
5. Fibumo Xavery Kivenule
6. Mlagile Anyesi Kivenule
7. John Kivenule
Bibi Nyanyilimale Singaile (Mke wa
Pili)
1. Mgulwa Agnes Kivenule
2. Luhanage Ponsiano Kivenule
3. Mgendwa Eusebio Kivenule
4. Msinziwa Daniel Kivenule
5. Kanolo Edward Kivenule
Mke wa Tatu wa Bibi Pangulimale
Setwanga
1. Conjeta Kivenule
2. Pyela Kivenule
3. Faustino Kivenule
4. George Kivenule
5. Carolina Kivenule
Babu Sigatambule Kivenule alifariki
mwaka 1995 na kuzikwa eneo la Mlafu, Kidamali - Iringa. Hali kadhalika mke wake
Mkubwa Bibi Siwangumhavi Singaile Mwilumbwa alifariki dunia mwaka 1999 na
kuzikwa eneo hilo hilo la Mlafu.
Mzee Hussein Tavimyenda Kivenule
alikuwa ni mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo. Yeye aliishi eneo la Ulefi na
baadaye Mlafu. Hatimaye alihamia Magubike. Babu Hussein Kivenule hadi anafariki
dunia Juni 26, 2013 anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 113 kwa mujibu wa
taarifa na tafiti ambazo tunazo.
Babu Hussein Tavimyenda Kivenule
ameshiriki kikamilifu katika Vita vya Pili ya Dunia. Wakati anashiriki vita
hiyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 44. Amepigana vita maeneo mbalimbali
mfano Burma, India na Ulaya. Kwa sasa ana upofu wa macho ambao anasema
ulisababishwa na Baruti. Hali kadhalika anakiri kuwa kuendelea kuwa hai ni kwa
sababu alipigana upande wa Mwingereza. Anakiri vita ndiyo iliyomsababishia
upofu pengine asingekuwa na hali aliyonayo kwa sasa.
Mzee Hussein Kivenule alioa wake wawili
na kubahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa mke wake wa kwanza Bibi
Yimilengeresa Semsisi. Babu Hussein alipata watoto wafuatao:
1. Nyakudila Benjamin Kivenule
2. Sekiyavile Modesta Kivenule
3. Dominicus Kivenule
4. Emmanuel Kivenule
5. Luciana Kivenule
6. Ajendina Kivenule
Kwa upande wa mke wa pili wa Bibi
Dalika Setala, Mzee Hussein Kivenule alipata watoto wafuatao:
1. Kabogo
Bernadi Kivenule
2. Sembata
Josephine Kivenule
3. Necia Kivenule
4. Batromeo Kivenule
5. Brandino Kivenule
6. Tavina Kivenule
7. Masikitiko Kivenule
Asilimia kubwa ya familia ya Babu
Hussein Kivenule inaishi maeneo ya Magubike, Idete na Ibogo. Pia wapenda
historia mnakaribishwa kwenda kumtembelea Babu Hussein Kivenule.
UZAO WA SALAMALENGA KAHENGULA KIVENULE
Babu Salamalenga Kahengula Kivenule
alikuwa ni mtoto pekee wa kiume wa Babu Kalasi kwa mke wake wa pili Bibi
Mnyamtage Sekindole. Kahengula pia ni kaka wa Bibi Mganga Semhumba, aliyekuwa
mtoto pekee kwa Mwamhumba, aliyefariki mara tu baada ya kumzaa Bibi Mganga kwa
Sekindole.
Babu Salamalenga Kahengula Kivenule
alio wake watatu ambao ni:
1. Bibi Semkonda
2. Bibi Semfilinge
3. Bibi Nyangali
Salamalenga anapomuoa Bibi Semkonda
alimkuta na mtoto wa kufikia Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi. Kwa wake
zake hawa watatu, Babu Salamalenga alibahatika kupata watoto kumi na tatu (13).
Kwa Bibi Semkonda alibahatika kupata watoto wafuatao:
1. Pangayena Kivenule
2. Jonas Kivenule
3. Samwel Kivenule
4. Galasamaneno Kivenule
5. Daud
(William) Kivenule
6. Barton Kivenule
Kwa mke wa pili Bibi Semfilinge, Babu
Salamalenga alizaa nae watoto watatu ambao ni:
1. Chogavanu Kivenule
2. Munguatosa Kivenule
3. Mwilimilisa Kivenule
Na kwa mke wa tatu Bibi Nyangali, Babu
Salamalenga alizaa nae watoto wanne (4) ambao ni:
1. Tindasulanga Kivenule
2. Sigongola Kivenule
3. Shaban Kivenule
4. Gungamesa Kivenule
MWINGILIANO NA KOO NYINGINE KATIKA
HIMAYA YA UHEHE
Zaidi ya Koo mbalimbali 50
zinachangamana na Ukoo wa Kivenule. Hii ni kutoka Karne ya 18 ambapo kizazi
hiki kilianza kujitambua na kujikusanya. Baadhi ya Koo ambazo zimechangamana na
ukoo huu ni pamoja na koo za:
1. Kabogo
2. Kamtawa
3. Katowo
4. Kigereso
5. Kindole
6. Kisumbe
7. Kiteve
8. Kitu
9. Kusiga
10. Lawa
11. Luhwavi
12. Lupola
13. Madembwe
14. Manimu
15. Matagi
16. Mdongwe
17. Mfilinge
18. Mhapa
19. Mhumba
20. Mkeng'e
21. Mkonda
22. Mnonikirwa
23. Mnyavanu
24. Msisi
25. Mtono
26. Mvemba
27. Myalla
28. Ngeng'ena
29. Ngolo
30. Ngwenga
31. Ngweta
32. Nyakunga
33. Nyangali
34. Nyangalima
35. Twanga
36. Nzala
37. Sambagi
38. Senosa
39. Setala
40. Singaile
41. Utenga
42. Kalinga
43. Sungu
44. Mgimwa
45. Nyamika
46. Nongele
Kwa taarifa na mawasiliano na:
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI)
http://www.tagumtwa-kivenule.blogspot.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni