Chimbuko la Ukoo = KAUKI

Chimbuko la Ukoo = KAUKI
KAUKI

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 14 WA KAUKI

Jumatano, 24 Aprili 2024

IJUE HISTORIA YA KAUKI


UTANGULIZI
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) ni sehemu ya harakati za Maendeleo zinazofanywa katika kujikwamua na kuondokana na matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii hii.

KAUKI hufanya mikutano kwa wanaukoo kama sehemu wa mwendelezo wa jitihada za namna hii ambayo imekuwa ikifanywa mara moja kila mwaka. Kwa mara kwanza katika historia, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika, tarehe 17 – 18 Desemba 2005, katika Ukumbi wa Sanga, Kijijini Kidamali, mkoani Iringa.

Umoja wa Ukoo wa Kivenule ulizinduliwa rasmi mwaka 2006, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika tarehe 24 – 25 Juni 2006 katika Ukumbi wa Sanga Kijijini Kidamali, Iringa.

Kuzinduliwa kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, kulienda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Ukoo pamoja na Kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule na hivyo kuwa Katiba Rasmi. Kuwepo kwa Katiba ya KAUKI kulitoa fursa ya kuanza kwa utekelezaji wa shughuli na mipango mbalimbali ya maendeleo.

Pia, pamoja na mambo mengine, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo, kulifanya uchaguzi wa Viongozi wa Kanda, uchaguzi wa Walezi wa Ukoo na hivyo utendaji rasmi wa KAUKI kuruhusiwa kuanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni