TANZIA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule
(KAUKI) unasikitika kutangaza kifo cha Mareh. ANNA VANULICHUMA NONGELE,
kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mnano tarehe 06 Septemba
2024, Jijini Dar es Salaam. Mareh. ANNA VANULICHUMA NONGELE ni Mama Mzazi wa
Mwenyekiti wa Ukoo Ndugu Onesmo Bernard Kivenule.
Mazishi ya Mareh. ANNA
VANULICHUMA NONGELE yamefanyika tarehe 08 Septemba 2024 Kijijini Magubike,
Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa.
Mareh. ANNA VANULICHUMA
NONGELE amekuwa akisumbuliwa na tatizo la Saratani toka mwezi Septemba 2023 na
amekuwa akiendelea na matibabu mpaka mauti yalipomfika. Raha ya Milele Umpe Ee
Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, apumzike kwa amani – Amina.
Mungu alitoa na leo ametwaa
Jina lake Lihimidiwe. Amina.
Imetolewa na:
Adam
Alphonce Kivenule
Katibu
Mkuu wa KAUKI

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni