TAARIFA YA UTENDAJI NA MAENDELEO YA KAUKI
KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Ni jina la Katiba ya Umoja huo, lililokubaliwa kutumika na wana-KAUKI katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, uliofanyika tarehe 24 na 25 Juni 2006, Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa. Katiba ya KAUKI tayari ilishaanza kutumika mara tu baada ya Mkutano Mkuu wa Pili. Nakala kadhaa za KAUKI tayari zimesambazwa na zinaendelea kutumika. Katiba ya KAUKI ni mwongozo wa shughuli mbalimbali zinazofanyika ndani na ikibidi kama kuna umuhimu nje ya KAUKI ili kuuletea maendeleo umoja huu.
KAUKI ina viongozi wa ngazi mbalimbali waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Pili. Viongozi hao wanajulikana kama Viongozi wa Kanda. Kila Kanda ambayo ilikubalika kuwepo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI, ina viongozi siyo zaidi ya mmoja.
Viongozi hawa, wanawajibika kwa wanaukoo wanaotoka katika maeneo yale wanayoishi. Wajibu na majukumu ya viongozi wa KAUKI yamebainishwa katika Katiba. Wajibu wao ni kushirikiana miongoni mwao pamoja na Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza masuala mbalimbali ya maendeleo yanayouhusu ukoo. Pia, ni wajibu wa viongozi hawa, kuwashauri Viongozi wa KAUKI katika masuala mbambali yanayoukabili ukoo wetu kwa mfano masuala ya ugonjwa, elimu, uchumi na maendeleo.
Viongozi wa Kanda wana nguvu ya Kikatiba katika kutimiza wajibu wao na pia wana wajibu wa kuhakikisha kuwa mipango mbalimbali inayopangwa kupitia Kamati Kuu au Mkutano Mkuu wa KAUKI inatekelezwa.
Viongozi wa ngazi nyingine za juu kama Katibu, Mwenyekiti, Makamu wa Katibu, Makamu wa Mwenyekiti, Mweka Hazina na Msaidizi wake, wana wajibu wa kuwahimiza viongozi wa Kanda, kushirikiana baina yao wenyewe na pia kushirikiana na viongozi wakuu kutekeleza wajibu na majukumu mbalimbali ambayo yanatukabili.
Kwa mujibu wa KAUKI, viongozi wa Kanda, wana wajibu kuhudhuria vikao mbalimbali kama inavyoainishwa kwenye Katiba ya KAUKI. Wajibu huo pia unawagusa viongozi wengine wa KAUKI na wanawajibika ipasavyo kutekeleza na kutimiza wajibu wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni