Chimbuko la Ukoo = KAUKI

Chimbuko la Ukoo = KAUKI
KAUKI

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 14 WA KAUKI

Jumatatu, 3 Mei 2010

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TANO WA KAUKI-JUNI 26-27, 2010


MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TANO WA KAUKI-JUNI 26-27, 2010
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Tano wa KAUKI, katika eneo la Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya KAUKI ambayo tayari imeshafanyika Kidamali mara mbili, Irole na Nduli. Mkutano Mkuu wa KAUKI umeazimia kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kufundisha mada mbalimbali; Kupeana na kujengeana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na maisha; Kupitia na kujadili michango mbalimbali ya maendeleo; Kujadili namna ya kudumisha kumbukumbu mbalimbali za wana-KAUKI; na Kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa KAUKI. Sambamba na Mkutano huu; taratibu za maandalizi zinafanyika toka pande zote za Dar es Salaam, Kidamali, Magubike, Irole, Nduli, Itagutwa na kwingineko ambako wana-KAUKI wanaishi. Mafanikio ya Mkutano Mkuu wa Tano wa KAUKI unategemea nguvu ya wana-KAUKI, ambayo inahusisha michango ya aina mbalimbali kama fedha taslimu, mazao, mifugo na pia kujitolea kwa hali na mali. Viwango vya michango vinatofautiana na kulinga na mahali na pia aina ya shughuli. Lakini kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, itabidi wana-KAUKI wakubaliane na viwango vipya vya michango. Kwa upande wa mijini, tunapendekeza kiwango cha shilingi elfu kumi (10,000.00) kiendelee kutumika na kwa upande wa vijijini, kiwango cha shilingi elfu sita 6,000.00 tu kitolewe. Fedha hizi zitasaidia katika kutoa huduma, mfano chakula, maji na huduma nyingine za msingi kuhakikisha kuwa mkutano unafanyika. Tunatoa changamoto na hamasa kwa wana-KAUKI kuwa macho katika kuhakikisha kuwa mkutano huu unafanyika.

Imetolewa na: Adam Kivenule Katibu wa KAUKI 0713 270364

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni