Chimbuko la Ukoo = KAUKI

Chimbuko la Ukoo = KAUKI
KAUKI

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 14 WA KAUKI

Jumapili, 23 Juni 2024

RATIBA YA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI - KIDAMALI , IRINGA

 

RATIBA YA SIKU MOJA YA MKUTANO MKUU WA KAUKI

KIDAMALI - IRINGA

29 Juni 2024

MUDA

SHUGHULI/JUKUMU

MHUSIKA

12.00-01.00

Asubuhi

Kuamka na Kujiandaa

Ndugu Wote

01.00-02.00

Kifungua Kinywa (Chai/Kahawa)

Ndugu Wote

02:00-03:00

Kujisajili na Kupata Vitambulisho

Washiriki Wote

03.00–03.15

Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI

Mwenyekiti wa KAUKI

03.15-03.30

Ufunguzi Rasmi wa Mkutano na Mgeni Rasmi

Mgeni Rasmi

03.30-04.00

Utambulisho wa Ndugu na Wageni Waalikuwa

Washiriki Wote

04.00-05:00

Mada: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO

1.      Washiriki wasambaziwe nakala ya muundo wa Ukoo na kasha kuujadili na kutoa mawazo yao

·         Mwakilishi – Kidamali

·         Mwakilishi - Ilole

·         Washiriki wote

05:00-05:30

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

05.30-07.00

Mchana

Mada Inaendelea.

2.      Washiriki waijadili mada na kutoa mapendekezo

3.      Washiriki waijadili mada na kupendekeza nini kifanyike kutunza kumbukumbu hizo

4.      Washiriki wazijadili njia mbadala za kutunza taarifa zinazohusiana na ukoo

Wawezeshaji na Washiriki wote

Majadiliano

Washiriki wote na Wawezeshaji

Majumuisho

Wawezeshaji

07.00-08.00

CHAKULA CHA MCHANA

Washiriki wote

08:00-08:40

TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI:

1.      Mipango na Shughuli zilizokusudiwa kufanywa na KAUKI 2017-2024;

2.      Taarifa ya Utendaji kwa Ujumla;

3.      Taarifa ya Mahesabu na Fedha; na

4.      Mafanikio na Matatizo ya KAUKI

5.      Matarajio ya KAUKI 2024/25

6.      Changamoto za KAUKI na Namna ya Kukabiliana nazo

1.      Katibu Mkuu

2.      Makamu wa Katibu

3.      Mhasibu

08.40 – 09.20

Alasiri

TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KANDA

1. HAMASA

2. CHANGAMOTO

3. MIKAKATI

4. MAFANIKIO

·         Viongozi wa Kanda zote

·         Ndugu toka Kanda Husika

9:20 – 9:45

HALI YA UKOO/KAUKI

Kujadili Mapungufu, Kutoa Ushauri, Mapendekezo

·         Katibu Mkuu

·         Katibu Msaidizi

·         Washiriki wote

09:45-10:00

Salaam mbalimbali kutoka kwa Washiriki wa Mkutano Mkuu (Wastani watu 6 na dakika @ 5)

Washiriki wa Mkutano

10.00-10:30

Jioni

Uzoefu wa wanaukoo katika shughuli za maendeleo

1.      Kidamali/Magubike: Kilimo cha Nyanya /Tumbaku na shughuli nyingine za kiuchumi dakika 25

2.      Ilole/Nduli/Kigonzile/Mgongo: Uzoefu wa Shughuli za Kiuchumi dakika 25

3.      Dar/ Morogoro/ Kilombero / Dodoma/Mafinga dakika 5

4.      Maeneo Mengine

Washiriki wote; viongozi wa Kanda au wajumbe watakaochaguliwa kutoa uzoefu wa shughuli hizo za kiuchumi

10.30-10:35

Kutaja Tarehe ya Mkutano Mwingine wa KAUKI

Kuahirisha Mkutano

 

10.35-10.45

KUAHIRISHA MKUTANO

Viongozi wa Dini

Kiongozi wa KAUKI

Mapumziko : Chai/Kahawa/Maji na Vinywaji

Washiriki wote

30 Juni 2024

MUDA

SHUGHULI/JUKUMU

MHUSIKA

12.00-02.00

Asubuhi

Kuamka na Kuhudhuria Ibada (Kanisani)

Ndugu Wote wa Dhehebu la Kikristo

02.00-03.00

Kifungua Kinywa (Chai/Kahawa)

Ndugu Wote

03:00-03:30

Kujisajili na Kupata Vitambulisho

Washiriki Wote

03.30–04.15

MADA:

Mtoa Mada

04.15-04.30

Mjadala Kuhusiana na Mada

Wote

04.30-05.30

MADA:

Mtoa Mada

05.30-06:30

Mchana

MADA:

Mtoa Mada

06.30-07.20

YATOKANAYO NA MKUTANO MKUU

1.      Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI

2.      Mipango na Mikakati ya KAUKI

3.      Tarehe ya Mkutano Mkuu wa 14 wa KAUKI

Viongozi

Wanaukoo

Majadiliano

Washiriki wote na Wawezeshaji

Majumuisho

Wawezeshaji

07.20-07.40

SALAAM TOKA KANDA MBALIMBALI

Washiriki wote

07:40-08:00

SALA

KUFUNGA MKUTANO

Viongozi wa Dini

Viongozi wa Ukoo

 

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA HARUSI YA MTOTO WA NDUGU ALEXANDER NYANGALIMA - DAR ES SALAAM - VIDEO

 



Ndugu Onesmo Bernard Kivenule na Bi. Glory Xavery Kivenule moja katika moment nzuri wakati wa Harusi ya Binti ya Mzee Alexander Nyangalima, Mjukuu wa Kwanza wa Sigatambule Tavimyenda Kivenule


MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA HARUSI YA MTOTO WA NDUGU ALEXANDER NYANGALIMA - DAR ES SALAAM

 

   Wa Nne kutoka kushoto ni Shangazi yetu Mama Neema kutoka Magubike Iringa


    Wa pili kutoka kushoto ni Mzee Brandino Hussein Kivenule, Mzee Athuman Mtono (Mtoto wa Sekivenule), Mzee Alexander Nyangalima (Mtoto wa Sekivenule) 




































Wa kwanza kushoto ni Ndugu Onesmo Bernard Kivenule na Dada Gloria Xavery Kivenule

Jumamosi, 22 Juni 2024

MAOMBI YA MCHANGO WA KUFANIKISHA MKUTANO WA 13 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)


 

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI

Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya Wanaukoo Wote; wanayofuraha kubwa kuwakumbusha kuwa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI unatarajia kufanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Juni 2024, Kijijini Kidamali, Mkoa wa Iringa. Mkutano huu ni Mwendelezo wa Mikutano ya Ukoo ambayo hufanyika kila Mwaka. 

Ili kufanikisha Mkutano huo, Wanaukoo Wote wanaombwa kutoa Michango yao ili kufanikisha Mkutano huo. Watu Wazima Watachangia Shilingi 10,000/- na Watoto 5,000/-. Michango hii itasaidia upatikanaji wa huduma za Chakula, Chai na Maji kwa Siku zote tutakazokuwa Kidamali. Michango itolewe kwa Viongozi wa Kanda Husika. 

Malengo ya Mkutano Mkuu ni pamoja na:

1.     Kutambulishana na Kufahamiana Ndugu/Wanaukoo;

2.     Kujua Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;

3.     Kubadilishana Taarifa na Uzoefu Mbalimbali wa Shughuli za Maisha;

4.     Kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha undugu na ushirikiano baina ya Wanaukoo; na mengineyo.

Mikutano ya KAUKI huhudhuriwa na Wanaukoo kutoka Maeneo ya Magubike, Kidamali, Kalenga, Nzihi, Nyamihuu, Nyamahana, Nduli, Mgongo, Itagutwa, Igominyi, Vilalo, Migoli, Iringa Mjini, Mafinga, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza na Maeneo mengine ambayo washiriki wanaishi.

Imeandaliwa na Kutolewa na:

Faustino Sigatambule Kivenule

Mwenyekiti wa Ukoo

Jumatano, 1 Mei 2024

VIONGOZI WA KAUKI KANDA YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, DODOMA NA MAFINGA WAWEKA MIKAKATI KABAMBE KWA AJILI YA KUFANIKISHA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI

VIONGOZI wa KAUKI toka Kanda za Dar es Salaam, Dodoma, MOROGORO na Mafinga, wamefanya kikao-mkakati kwa ajili ya kufanikisha Mkutano wa 13 WA KAUKI, utakaofanyika Kijijini Kidamali… Mkutano huo utafanyika tarehe 29 Juni 2024.

 Taarifa zaidi zitatolewa ikiwemo Mapendekezo ya Bajeti.

Nawapongeza wote walioshiriki katika kikao hicho. 

Asante