Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya Wanaukoo Wote; wanayofuraha kubwa kuwakumbusha kuwa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI unatarajia kufanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Juni 2024, Kijijini Kidamali, Mkoa wa Iringa. Mkutano huu ni Mwendelezo wa Mikutano ya Ukoo ambayo hufanyika kila Mwaka.
Ili kufanikisha Mkutano huo, Wanaukoo Wote
wanaombwa kutoa Michango yao ili kufanikisha Mkutano huo. Watu Wazima
Watachangia Shilingi 10,000/- na Watoto 5,000/-. Michango hii itasaidia
upatikanaji wa huduma za Chakula, Chai na Maji kwa Siku zote tutakazokuwa
Kidamali. Michango itolewe kwa Viongozi wa Kanda Husika.
Malengo ya Mkutano Mkuu ni pamoja na:
1. Kutambulishana na Kufahamiana
Ndugu/Wanaukoo;
2. Kujua Chimbuko na Historia ya
Ukoo wa Kivenule;
3. Kubadilishana Taarifa na Uzoefu
Mbalimbali wa Shughuli za Maisha;
4. Kuweka mikakati mbalimbali ya
kuimarisha undugu na ushirikiano baina ya Wanaukoo; na mengineyo.
Mikutano ya KAUKI huhudhuriwa na Wanaukoo kutoka
Maeneo ya Magubike, Kidamali, Kalenga, Nzihi, Nyamihuu, Nyamahana, Nduli,
Mgongo, Itagutwa, Igominyi, Vilalo, Migoli, Iringa Mjini, Mafinga, Dar es
Salaam, Morogoro, Mwanza na Maeneo mengine ambayo washiriki wanaishi.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Faustino Sigatambule Kivenule
Mwenyekiti wa Ukoo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni