Chimbuko la Ukoo = KAUKI

Chimbuko la Ukoo = KAUKI
KAUKI

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 14 WA KAUKI

Jumatatu, 26 Mei 2025

RATIBA YA MKUTANO MKUU WA 14 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)


https://tagumtwa-kivenule.blogspot.com/

RATIBA YA MKUTANO MKUU WA 14 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)-KIDAMALI - IRINGA

Siku ya Kwanza: JUMAMOSI  21 JUNI 2024

MUDA

SHUGHULI/JUKUMU

MHUSIKA

12.00-01.00 Asb.

Kuamka na Kujiandaa

Ndugu/Wanaukoo Wote

01.00-02.00

Kupata Kifungua Kinywa (Chai/Kahawa/Uji)

·         Ndugu Wote

·         Kamati ya Maandalizi

02:00-02:50

1.      Kukaribisha Wageni

2.      Kujisajili/Orodhesha Washiriki

3.      Kuwapa Vitambulisho

·         Kamati ya Maandalizi

·         Washiriki Wote

02:50-02:55

Dua/Sala ya Kuombea Mkutano

·         Viongozi wa Dini

02:55-03:00

Salaam toka Kanda ya Kidamali: Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu 14 wa KAUKI

·         Mwakilishi Kanda ya Kidamali

03.00–03.05

Neno fupi la Kumkaribisha na Kumtambulisha Mgeni Rasmi

·         Mwenyekiti wa KAUKI

03.05-03.25

Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI

·         Mgeni Rasmi

03.25-04.00

Utambulisho wa Ndugu na Wageni Waalikuwa

·         Mwenyekiti-KAUKI

·         Washiriki Wote

04.00-05:00

MADA: Chimbuko/Asili Na Historia Ya Ukoo Wa Kivenule

1.      Mjadala: Muundo wa Ukoo wa Ukoo wa Kivenule (Nakala Zisambazwe)

·         Mtoa Mada

·         Viongozi-KAUKI

·         Washiriki wote

05:00-05:30

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

05.30-07.00

Mchana

Mada Inaendelea

2.      Namna ya Kuiboresha Mada: Mapendekezo

3.      Nini kifanyike kutunza kumbukumbu za Ukoo

4.      Njia Mbadala za Kutunza Taarifa za Ukoo

·         Viongozi-KAUKI

·         Wawezeshaji

·         Washiriki wote

Majumuisho

·         Viongozi wa KAUKI

07.00-08.00

CHAKULA CHA MCHANA

Washiriki wote

08:00-08:40

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KANDA

Nafasi:

1.      Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti

2.      Katibu na Naibu Katibu

3.      Mweka Hazina/ Walezi wa Kanda, Wahamasishaji

1.      Kanda ya DAR

2.      Kidamali/Magubike

3.      Kalenga/Irore

4.      Nduli/Morogoro

5.      Dodoma/Mafinga

08.40 – 09.20

Alasiri

Maendeleo ya KAUKI Katika Kanda:

1.      Hamasa, Mafanikio

2.      Changamoto na Mikakati

·         Viongozi wa Kanda

·         Ndugu toka Kanda Husika

9:20 – 9:45

Hali ya Ukoo/KAUKI: Maendeleo kwa Ujumla;Changamoto;Ushauri na Mapendekezo

·         Viongozi wa KAUKI

·         Wanaukoo Wote

09:45-10:00

Salaam mbalimbali kwenye Mkutano Mkuu 14 wa KAUKI (Wastani watu 6 @ dakika 2)

·         Washiriki wa Mkutano

10.00-10.45

Jioni

Kuahirisha  Mkutano hadi

Siku ya Jumapili tarehe 21 Juni 2025

·         Mwenyekiti – KAUKI

·         Washiriki Wote

02:00 - 06:00   

Usiku

NDUGU KUJUMUIKA PAMOJA (KAUKI NIGHT GALA) kwa ajili ya Vinywaji na Nyama Choma

Ndugu Wote

Kamati ya Maandalizi

   

RATIBA YA MKUTANO MKUU WA 14 WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)-KIDAMALI - IRINGA

Siku ya Pili: JUMAPILI  22 JUNI 2024

MUDA

SHUGHULI/JUKUMU

MHUSIKA

12.00-01.00 Asb.

Kuamka na Kujiandaa kwenda Kanisani

Ndugu Wote

04.00-05.00

Kupata Kifungua Kinywa (Chai/Kahawa/Uji)

·         Ndugu Wote

·         Kamati ya Maandalizi

05:00-06:00

MADA YA II: ELIMU YA UJASILIAMALI - 1

·         Uwasilishaji

·         Mjadala

·         Majumuisho

·         Mwezeshaji

·         Washiriki Wote

06:00-07:00

MADA YA III: ELIMU YA UJASILIAMALI - 2

·         Uwasilishaji

·         Mjadala

·         Majumuisho

·         Mwezeshaji

·         Washiriki Wote

07:00-08:00

MAPUMZIKO YA CHAKULA CHA MCHANA

·         Washiriki Wote

08.00–09.00

Alasiri

MADA YA IV: ELIMU YA UJASILIAMALI - 3

·         Uwasilishaji

·         Mjadala

·         Majumuisho

·         Mwezeshaji

·         Washiriki Wote

09.00-09.30

·         Majumuisho ya Mkutano Mkuu wa 14 wa KAUKI

·         Maazimio

·         Viongozi wa KAUKI

·         Washiriki Wote

09.30-09.40

·         Neo la Shukrani Toka Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 14 wa KAUkI - Kanda Ya Kidamali

·         Mwenyekiti  wa Kamati ya Maandalizi

09.40-09:50

Neno la Shukrani toka kwa Viongozi wa KAUKI

·         Viongozi wa KAUKI

09:50-09:55

KUTANGAZA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA 15 WA KAUKI NA MAHALI UTAKAPOFANYIKIA

·         Mwenyekiti – KAUKI

·         Washiriki Wote

09:55.00-10.00

Jioni

Kuahirisha  Mkutano Mkuu wa KAUKI  - 2025

·         Mwenyekiti – KAUKI

 

10:00

MWISHO

Ndugu Wote

Kamati ya Maandalizi

 


Jumatatu, 4 Novemba 2024

CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE

Utangulizi

Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule (KAUKI) iliwasilishwa na Mzee William Sigatambule Kivenule. Mwasilishaji wa Mada ni Mzee wa Heshima katika Ukoo wa Kivenule ni Tunu kwa sababu ana madini ya kutosha kuhusiana na masuala ya Ukoo wa Kivenule. KAUKI imekuwa ikimtumia katika Mikutano yake Kuwasilisha Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule.

Katika Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI, Mzee Wiliam Sigatambule Kivenule aliwasilisha Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule.  Mwasilishaji wa Mada alianza kwa kuelezea kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule; huku akielezea kwa kina waanzilishi wa Ukoo wa Mwibalama. Mtoa Mada alisema kuwa Ukoo wa Kivenule awali haukuitwa hivyo, uliitwa MWIBALAMA. Kivenule kwa Asili ni akina Balama ni ndugu wa Karibu kabisa ambao hawapaswi hata kuoana.

Picha ya Mzee William Sigatambule Kivenule wa kwanza kutoka kushoto ndiye aliyewasilisha Mada ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule katika Mkutano Mkuu wa KAUKI (2024)

CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE

Historia ya Chimbuko la Ukoo wa Kivenule limetoka mbali zaidi hata kabla ya Jina la sasa la KIVENULE kupatikana. Utafiti unaoendelea kufanyika kila mwaka umesaidia kuboresha Chimbuko la Ukoo wa Kivenule.









Picha inaonesha Vitabu vya Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule vilivyoganywa wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI – Kidamali, Iringa 29 – 30 Juni 2024

Chanzo: KAUKI - 2024

Waanzilishi Sita (6) wa Ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA)

Kwa mujibu wa Mzee Wiliam Sigatambule Kivenule, wapo Watoto Sita ndio waliopelekea kuanzishwa kwa Ukoo wa Balama. Vizazi hivyo vya akina Balama vilikuja Kumzaa Tagumtwa BALAMA ambaye baadaye ndiye aliyeleta ukoo wa Kivenule. Chimbuko la Mwibalama ni pale Malangali ambayo ipo Kusini mwa Mufindi, katika Mkoa wa Iringa.

Tafiti za sasa zilizopatikana kupitia Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI zinaonesha kuwa BABU------------- ndiye aliyemzaa BABU MWIGINGILI BALAMA; BABU MWIGINGILI BALAMA ndiye alimzaa BABU MNYARUNGEMBA BALAMA; BABU MNYARUNGEMBA BALAMA ndiye aliyemzaa BABU NYAKUDILA BALAMA; BABU NYAKUDILA BALAMA ndiye aliyemzaa BABU KANOLO BALAMA;  BABU KANOLO BALAMA ndiye aliyemzaa BABU MTENGILINGOMA BALAMA; na BABU MTENGILINGOMA BALAMA akamzaa BABU TAGUMTWA BALAMA.























Picha 2: hazina ya Mashangazi (Sekivenule) kama ilivyochukuliwa katika moja ya matukio yaliyowakutanisha Wanaukoo. Wa pili toka kushoto ni Katibu Mkuu wa Ukoo wa KivenuleChanzo: KAUKI - 2024 

Mababu wote hawa tunaowazungumza hapa chini ni Waanzilishi wa UKOO WA BALAMA (akina MWIBALAMA) na Baadaye UKOO WA KIVENULE.





Maelezo haya yote tunayoyazungumzia ni katika Karne ya 17 kabla ya kuja kwa BABU TAGUMTWA BALAMA, ambaye aliuleta Jina la KIVENULE. BABU MTENGELINGOMA BALAMA ndiye Baba Mzazi wa TAGUMTWA BALAMA.

Wakati huu Babu Tagumtwa Balama alikuwa hajaenda kwenye Vita za LIGALU.




Jumamosi, 28 Septemba 2024

TANZIA

 


TANZIA

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) unasikitika kutangaza kifo cha Mareh. ANNA VANULICHUMA NONGELE, kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mnano tarehe 06 Septemba 2024, Jijini Dar es Salaam. Mareh. ANNA VANULICHUMA NONGELE ni Mama Mzazi wa Mwenyekiti wa Ukoo Ndugu Onesmo Bernard Kivenule.

Mazishi ya Mareh. ANNA VANULICHUMA NONGELE yamefanyika tarehe 08 Septemba 2024 Kijijini Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa.

Mareh. ANNA VANULICHUMA NONGELE amekuwa akisumbuliwa na tatizo la Saratani toka mwezi Septemba 2023 na amekuwa akiendelea na matibabu mpaka mauti yalipomfika. Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, apumzike kwa amani – Amina.

Mungu alitoa na leo ametwaa Jina lake Lihimidiwe. Amina.

 

Imetolewa na:

 

Adam Alphonce Kivenule

Katibu Mkuu wa KAUKI

Jumapili, 30 Juni 2024

MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI WAFANYIKA KIDAMALI - IRINGA

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) umefanya Mkutano Mkuu wa 13 katika Kijiji cha Kidamali Mkoani Iringa. Mkutano huo umefanyika mnamo tarehe 29 – 30 Juni 2024, huku ukihudhuriwa na ndugu na wanaukoo zaidi ya 70 wakiwa na Vitambulisho vyao.

Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI unafanyika kwa mara nyingine baada ya Mkutano Mkuu wa Mwisho wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika katika Kijiji cha Vilalo, Irore Mkoani Iringa.

Baadhi ya Wanaukoo wa Kivenule waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI, Kidamali - Iringa


Mahudhurio ya Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI hayakuwa ya Kuridhisha kutokana na baadhi ya Kanda kutokuwa na Uwakilishi. Kanda ya Kidamali, Magubike, Dar eS Salaam, Mafinga, Morogoro, Iringa Mjini na Kalenga ndizo zilizokuwa na Uwakilishi katika Mkutano huo. Kanda za Nduli, Mgongo, Itagutwa, Igominyi na Vilalo hawakuhudhuria Mkutano kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika.

Mojawapo ya mambo makubwa yaliyofanyika katika Mkutano huo ni pamoja na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa KAUKI watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka 3 kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI.

Hali kadhalika Mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa Wanaukoo zikiwa na lengo la kuwajengea uwezo na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanaukoo.

Mkutano wa KAUKI wa 13 pia ulijadili changamoto mbalimbali zinazoukabili ukoo wa Kivenule na namna ya kuweza kuzitatua. Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya ardhi baina ya Ukoo wa Kivenule na Mwekezaji, ambao ulichukua sehemu kubwa ya ardhi. Mgogoro ardhi unaligusa eneo la Ulefi na eneo la Magubike, ambapo haya maeneo yaliyotwaliwa na Mwekezaji yalikuwa chini ya Umiliki wa Ukoo wa Kivenule na hata ushahidi wa Makaburi ya Waasisi wa Ukoo yapo kwenye hiyo ardhi iliyotwaliwa.

Mzee Bernard Hussein Kivenule akiwa na Dada zake wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI - Kidamali Iringa.

Changamoto nyingine kuzorota kwa mahusiano baina ya Wanaukoo na kutofanyika kwa Mikutano ya KAUKI toka mwaka 2017.

Pia Mkutano huo ulikuja na mpango madhubuti wa ukusanyaji wa michango na pia kuendelea kuboresha Mikutano Mikuu ya Ukoo ya Kivenule.

Wanaukoo wote kwa pamoja walikubaliana kwamba wataanza kutumia M-Koba kama njia madhubuti ya Ukusanyaji na Utunzaji wa Fedha za Michango toka kwa Wanaukoo.


Usiku wa Chakula Maalum kwa Wanaukoo - kilichofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI

Jumla ya Ahadi ya Shilingi Milioni 1,250,000 zilipatikana kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 14 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Kidamali. Aidha kiasi cha shilingi 130,000/-  taslimu zilipatikana wakati wa Mkutano huo ikiwa ni michango iliyotokana na ahadi toka kwa Wanaukoo kwa ajili ya Mkutano Mkuu Ujao wa KAUKI.

MABORESHO KATIKA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI

Moja ya eneo lililoboreka kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ni kuongezeka kwa Bajeti ya Mkutano na pia Wanaukoo kuwa katika Mavazi rasmi ya Mkutano huo. Wanaukoo wa Kanda ya Dar es Salaam, Dodoma, Mafinga na Morogoro walijitoa kwa hali na Mali kwa lengo la kufanikisha Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI. Hii ndiyo sababu ya kuboreka kwa bajeti ya Mkutano huo.

Mkutano wa 13 wa KAUKI uliandaa Usiku Maalum kwa Wanaukoo – Dinner Night Gala kwa Wanaukoo ambapo walijumuika pamoja, kunywa, kula na kubadilishana mawazo. Hili likuwa ni tukio adhimu ambalo lilikuwa halijawahi kutokea katika Mkutano wowote wa KAUKI.

Wanaukoo wakiwa katika Vazi la Tshirt Maalum zenye Nembo ya KAUKI waliupendezesha Mkutano Mkuu wa 13. Tshirt zenye rangi ya Kijivu, Nyeupe, Bluu na Rangi ya Damu ya Mzee zilivaliwa na Wanaukoo na Kuupamba Mkutano.

Imeandaliwa na:

 

Adam Alphonce Kivenule

Katibu Mkuu - KAUKI

Jumamosi, 29 Juni 2024

UKOO WA KIVENULE WAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAKE

 


KAUKI YAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) umefanya Uchaguzi wa Viongozi wake. Uchaguzi huu umefanyika leo Kidamali, Iringa wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ukoo.

Uchaguzi huo umehusisha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Ukoo, Makamu wa Mwenyekiti wa Ukoo, Katibu Mkuu wa Ukoo, Makamu wake, Mweka Hazina na Walezi wa KAUKI.

Waliochaguliwa kushika nyadhifa hizo ni pamoja na:

1.    Ndugu Onesmo Bernard Kivenule aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Ukoo

2.    Bi. Gloria Xavery Kivenule ambaye amechaguliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Ukoo

3.    Ndugu Adam Alphonce Kivenule aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ukoo,

4.    Ndugu Christian John Kivenule aliyechaguliwa kuwa Katibu Msaidizi

5.    Ndugu Lesandu Peter Mhapa aliyechaguliwa kuwa Mweka Hazina wa Ukoo; na:

Waliochaguliwa kuwa Walezi wa Ukoo Ukoo wa

6.    Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule

7.    Ndugu Vitus Nzala na

8.    Bi. Irene Kivenule  Kivenule.

Jumapili, 23 Juni 2024

DOKOZE KUTOKA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE - KAUKI

 

VIONGOZI WA KAUKI WASISITIZA UMUHIMU WA KUSHIRIKI KATIKA MISIBA YA NDUGU/WANAUKOO

Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) walifanya mazungumzo kuhusu umuhimu wa ndugu/wanaukoo kushirikiana katika misiba na raha. Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Ukoo wa Kivenule Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule alielezea kuhusu taratibu zinazotumika maeneo mbalimbali kuhusu uratibu na ushiriki katika misiba ya ndugu/wanaukoo.

Mwenyekiti alifafanua kuwa jukumu la kuratibu, kushiriki na kusimamia shughuli za misiba hubebwa na ndugu/wanaukoo waliopo katika eneo ambalo msiba unakuwa umetokea. Ndugu/Wanaukoo toka maeneo mengine, jukumu lao ni kusaidia kufanikisha shughuli za msiba huo. Kwa muktadha huo, hata viwango vya ushiriki katika msiba husika hutofautiana na wahusika waliopo eneo ambako kuna msiba. Lakini bado wajibu wa kuhakikisha shughuli zinazohusiana na msiba zinafanikiwa ni za kila ndugu/mwanaukoo.

Jambo la muhimu kuzingatia ni ushiriki wa ndugu/wanaukoo katika matukio yote ya misiba ya ndugu/wanaukoo; tofauti inayokuwepo ni viwango vya michango ya rambirambi ili kuweza kufanikisha mazishi ya msiba husika.

Kila maeneo wanatenga viwango vya michango ya rambirambi kwa msiba unaokuwa umetokea katika eneo husika. Pia kuna viwango vya michango kwa ajili ya misiba ambayo inakuwa imetokea mbali na maeneo ambayo msiba unakuwa unakuwa umetokea.

Basi tunasisitiza kuwa ni lazima tushiriki katika misiba yote, ila viwango vitatofautiana kwa misiba ambayo inakuwa imetokea maeneo yetu tunayoishi na ile ambayo imetokea maeneo ambayo hatuishi, lakini tuna wajibu wa kushiriki kwa hali na mali.

Hii itasaidia kupunguza mzigo wa michango kwa sababu kuna wakati kunakuwa na mfululizo wa misiba…kitu ambacho kinaweza kuwafanya ndugu washindwe kumudu.

Kwa hiyo, tunaweza kupendekeza viwango vya michango kwa misiba iliyotokea maeneo ya mbalimbali na tunapaswa kutoa rambirambi zetu.

Kwa ndugu wote tunaoishi Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mafinga, Mwanza na maeneo mengine tunapaswa kutoa rambirambi kwa msiba uliotokea Magubike. Tutoe chochote kwa kadri Mungu atakavyokuwa ametujalia.

Suala la Jingine lilikuwa kwenye mjadala ni ushiriki wa misiba kwa ndugu/wanaukoo. Tulilizungumzia suala la ndugu wengi waliopo Dar es Salaam na maeneo mengine tofauti na maeneo ya kwetu ambao wana jukumu la kushirikiana nasi katika shida na raha. Suala la kwenda kwenye misiba maeneo yote, kwa maana ya Iringa (Nduli, Irore, Kidamali, Magubike, Mufindi, Kalenga, Igominyi, Ilula na kwingineko ambako ndugu wanaishi) ni muhimu sana kwa kila ndugu/mwanaukoo.

Mwenyekiti alisisitiza umuhimu wa kuwatambua wanaukoo wote na kuwashirikisha. Pia alipendekeza vikao vya Wanaukoo vitakavyofanyika mwezi huu Oktoba 2023, ndugu/wanaukoo waelezwe wazi umuhimu wa kushiriki katika matatizo ya ukoo. Hata wale ambao tayari wana vikundi vyao watueleze wazi kuwa wao wataendelea kushiriki kupitia vikundi vyao…au watashiriki pande zote. Hili ni eneo ambalo pia litakuwa sehemu ya mjadala. Tunaomba ushiriki wa ndugu/wanaukoo uwe mkubwa.

Kikao kwa upande wa Dar es Salaam kimepangwa kufanyika tarehe 14 Oktoba 2023….Onesmo Bernard Kivenule atatupatia mwongozo wa wapi kikao kitafanyika.  

Kifupi ni haya ambayo yamekuwa sehemu ya mujadala.

Nawasilisha.

Asante

Imetolewa leo tarehe 02 Oktoba 2023