|
VIONGOZI WA KAUKI WASISITIZA UMUHIMU WA KUSHIRIKI KATIKA MISIBA YA NDUGU/WANAUKOO |
|
Viongozi wa Umoja wa Ukoo
wa Kivenule (KAUKI) walifanya mazungumzo kuhusu umuhimu wa ndugu/wanaukoo
kushirikiana katika misiba na raha. Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa
Ukoo wa Kivenule Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule alielezea kuhusu
taratibu zinazotumika maeneo mbalimbali kuhusu uratibu na ushiriki katika
misiba ya ndugu/wanaukoo. Mwenyekiti alifafanua
kuwa jukumu la kuratibu, kushiriki na kusimamia shughuli za misiba hubebwa na
ndugu/wanaukoo waliopo katika eneo ambalo msiba unakuwa umetokea.
Ndugu/Wanaukoo toka maeneo mengine, jukumu lao ni kusaidia kufanikisha
shughuli za msiba huo. Kwa muktadha huo, hata viwango vya ushiriki katika
msiba husika hutofautiana na wahusika waliopo eneo ambako kuna msiba. Lakini
bado wajibu wa kuhakikisha shughuli zinazohusiana na msiba zinafanikiwa ni za
kila ndugu/mwanaukoo. Jambo la muhimu
kuzingatia ni ushiriki wa ndugu/wanaukoo katika matukio yote ya misiba ya
ndugu/wanaukoo; tofauti inayokuwepo ni viwango vya michango ya rambirambi ili
kuweza kufanikisha mazishi ya msiba husika. Kila maeneo wanatenga
viwango vya michango ya rambirambi kwa msiba unaokuwa umetokea katika eneo
husika. Pia kuna viwango vya michango kwa ajili ya misiba ambayo inakuwa
imetokea mbali na maeneo ambayo msiba unakuwa unakuwa umetokea. Basi tunasisitiza kuwa ni
lazima tushiriki katika misiba yote, ila viwango vitatofautiana kwa misiba
ambayo inakuwa imetokea maeneo yetu tunayoishi na ile ambayo imetokea maeneo
ambayo hatuishi, lakini tuna wajibu wa kushiriki kwa hali na mali. Hii itasaidia kupunguza
mzigo wa michango kwa sababu kuna wakati kunakuwa na mfululizo wa misiba…kitu
ambacho kinaweza kuwafanya ndugu washindwe kumudu. Kwa hiyo, tunaweza
kupendekeza viwango vya michango kwa misiba iliyotokea maeneo ya mbalimbali
na tunapaswa kutoa rambirambi zetu. Kwa ndugu wote tunaoishi
Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mafinga, Mwanza na maeneo mengine tunapaswa
kutoa rambirambi kwa msiba uliotokea Magubike. Tutoe chochote kwa kadri Mungu
atakavyokuwa ametujalia. Suala la Jingine lilikuwa
kwenye mjadala ni ushiriki wa misiba kwa ndugu/wanaukoo. Tulilizungumzia
suala la ndugu wengi waliopo Dar es Salaam na maeneo mengine tofauti na
maeneo ya kwetu ambao wana jukumu la kushirikiana nasi katika shida na raha.
Suala la kwenda kwenye misiba maeneo yote, kwa maana ya Iringa (Nduli, Irore,
Kidamali, Magubike, Mufindi, Kalenga, Igominyi, Ilula na kwingineko ambako
ndugu wanaishi) ni muhimu sana kwa kila ndugu/mwanaukoo. Mwenyekiti alisisitiza
umuhimu wa kuwatambua wanaukoo wote na kuwashirikisha. Pia alipendekeza vikao
vya Wanaukoo vitakavyofanyika mwezi huu Oktoba 2023, ndugu/wanaukoo waelezwe
wazi umuhimu wa kushiriki katika matatizo ya ukoo. Hata wale ambao tayari
wana vikundi vyao watueleze wazi kuwa wao wataendelea kushiriki kupitia
vikundi vyao…au watashiriki pande zote. Hili ni eneo ambalo pia litakuwa
sehemu ya mjadala. Tunaomba ushiriki wa ndugu/wanaukoo uwe mkubwa. Kikao kwa upande wa Dar
es Salaam kimepangwa kufanyika tarehe 14 Oktoba 2023….Onesmo Bernard Kivenule
atatupatia mwongozo wa wapi kikao kitafanyika. Kifupi ni haya ambayo
yamekuwa sehemu ya mujadala. Nawasilisha. Asante Imetolewa leo tarehe 02
Oktoba 2023 |

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni