Umoja wa
Ukoo wa Kivenule (KAUKI) umefanya Mkutano Mkuu wa 13 katika Kijiji cha Kidamali
Mkoani Iringa. Mkutano huo umefanyika mnamo tarehe 29 – 30 Juni 2024, huku
ukihudhuriwa na ndugu na wanaukoo zaidi ya 70 wakiwa na Vitambulisho vyao.
Mkutano
Mkuu wa 13 wa KAUKI unafanyika kwa mara nyingine baada ya Mkutano Mkuu wa
Mwisho wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika katika Kijiji cha Vilalo, Irore Mkoani
Iringa.
Baadhi ya Wanaukoo wa Kivenule waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI, Kidamali - Iringa
Mahudhurio
ya Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI hayakuwa ya Kuridhisha kutokana na baadhi ya
Kanda kutokuwa na Uwakilishi. Kanda ya Kidamali, Magubike, Dar eS Salaam,
Mafinga, Morogoro, Iringa Mjini na Kalenga ndizo zilizokuwa na Uwakilishi
katika Mkutano huo. Kanda za Nduli, Mgongo, Itagutwa, Igominyi na Vilalo
hawakuhudhuria Mkutano kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika.
Mojawapo
ya mambo makubwa yaliyofanyika katika Mkutano huo ni pamoja na kufanyika kwa Uchaguzi
Mkuu wa Viongozi wa KAUKI watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka 3 kwa
mujibu wa Katiba ya KAUKI.
Hali
kadhalika Mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa Wanaukoo zikiwa na lengo la
kuwajengea uwezo na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili
wanaukoo.
Mkutano
wa KAUKI wa 13 pia ulijadili changamoto mbalimbali zinazoukabili ukoo wa
Kivenule na namna ya kuweza kuzitatua. Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya
ardhi baina ya Ukoo wa Kivenule na Mwekezaji, ambao ulichukua sehemu kubwa ya
ardhi. Mgogoro ardhi unaligusa eneo la Ulefi na eneo la Magubike, ambapo haya
maeneo yaliyotwaliwa na Mwekezaji yalikuwa chini ya Umiliki wa Ukoo wa Kivenule
na hata ushahidi wa Makaburi ya Waasisi wa Ukoo yapo kwenye hiyo ardhi
iliyotwaliwa.
Mzee Bernard Hussein Kivenule akiwa na Dada zake wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI - Kidamali Iringa.
Changamoto
nyingine kuzorota kwa mahusiano baina ya Wanaukoo na kutofanyika kwa Mikutano
ya KAUKI toka mwaka 2017.
Pia
Mkutano huo ulikuja na mpango madhubuti wa ukusanyaji wa michango na pia kuendelea
kuboresha Mikutano Mikuu ya Ukoo ya Kivenule.
Wanaukoo
wote kwa pamoja walikubaliana kwamba wataanza kutumia M-Koba kama njia
madhubuti ya Ukusanyaji na Utunzaji wa Fedha za Michango toka kwa Wanaukoo.
Usiku wa Chakula Maalum kwa Wanaukoo - kilichofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI
Jumla ya
Ahadi ya Shilingi Milioni 1,250,000 zilipatikana kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa
14 wa KAUKI, utakaofanyika Kijijini Kidamali. Aidha kiasi cha shilingi 130,000/-
taslimu zilipatikana wakati wa Mkutano
huo ikiwa ni michango iliyotokana na ahadi toka kwa Wanaukoo kwa ajili ya
Mkutano Mkuu Ujao wa KAUKI.
MABORESHO KATIKA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI
Moja ya
eneo lililoboreka kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ni kuongezeka kwa
Bajeti ya Mkutano na pia Wanaukoo kuwa katika Mavazi rasmi ya Mkutano huo.
Wanaukoo wa Kanda ya Dar es Salaam, Dodoma, Mafinga na Morogoro walijitoa kwa
hali na Mali kwa lengo la kufanikisha Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI. Hii ndiyo
sababu ya kuboreka kwa bajeti ya Mkutano huo.
Mkutano
wa 13 wa KAUKI uliandaa Usiku Maalum kwa Wanaukoo – Dinner Night Gala kwa
Wanaukoo ambapo walijumuika pamoja, kunywa, kula na kubadilishana mawazo. Hili
likuwa ni tukio adhimu ambalo lilikuwa halijawahi kutokea katika Mkutano wowote
wa KAUKI.
Wanaukoo
wakiwa katika Vazi la Tshirt Maalum zenye Nembo ya KAUKI waliupendezesha
Mkutano Mkuu wa 13. Tshirt zenye rangi ya Kijivu, Nyeupe, Bluu na Rangi ya Damu
ya Mzee zilivaliwa na Wanaukoo na Kuupamba Mkutano.
Imeandaliwa
na:
Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI